Kurekebisha mwelekeo wa Qiblah ndani ya swalah

Swali: Kuna kundi la watu waliswali makosa kinyume na Qiblah na wakajua hilo baada ya kupita muda wa swalah. Je, wairudie?

Jibu: Ikiwa ni upindaji mdogo haudhuru. Na ikiwa upindaji ni mkubwa wanalazimika kuirudia.

Swali: Vipi ikiwa watapinda katikati ya swalah na wakarekebisha mwelekeo wao?`

Jibu: Ikiwa ni upindaji mdogo na wakarekebisha inatosha.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22191/ما-حكم-من-صلى-لغير-القبلة-ثم-علم-بذلك
  • Imechapishwa: 05/11/2022