Vipi kuoanisha umasikini wa Mu´aawiyah na mahimizo ya kumuozesha aliye na dini na tabia?

Swali: Faatwimah bint Qays (Radhiya Allaahu ´anhaa) wakati alipomuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba Mu´aawiyah amemchumbia ambapo akamwambia:

”Ni mtu fakiri asiyekuwa na kitu.”

Maneno haya hayapingani na Hadiyth isemayo:

”Atapokujieni ambaye mnamridhia tabia na dini yake basi muozesheni.”?

Jibu: Hapana, ni kwa minajili ya nasaha. Faatwimah alimuomba ushauri Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akamjibu:

”Ni fakiri hana mali yoyote.”

Ni jambo linaweza kumdhuru kitendo cha kutokuwa kwake na mali.

”Abu Jahm haitoi fimbo yake kutoka begani.”

Bi maana anawapiga sana wanawake.  

Yule mwenye kutakwa ushauri ni mwenye kuaminiwa. Anatakiwa kutoa ushauri kwa yale anayoyajua na kufanya hivo hakuitwi usengenyi wala ghushi.

Swali: Kitendo cha mtu kuwa ni fakiri hana mali inahesabika ni aibu?

Jibu: Hapana. Maana yake ni kwamba hana kitu cha kumuhudumia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22309/حكم-التنبيه-على-عيوب-المتقدم-لخطبة-امراة
  • Imechapishwa: 02/02/2023