Mswaliji amepitwa na Rak´ah na imamu akasimama katika Rak´ah ya tano

Swali: Maamuma amejiunga na imamu katika Rak´ah ya pili na baadaye imamu akasimama katika Rak´ah ya tano pasi na kuzinduliwa. Maamuma akaingiwa na shaka. Wakati imamu alipomaliza Rak´ah ya tano ndipo akazinduliwa ambapo akasujudu sijda ya kusahau. Wakati alipokuwa katika hali hiyo ya kusujudu maamuma yule akasimama ili alipe Rak´ah moja.

Jibu: Asujudu sijda ya kusahau baada ya kulipa kile kilichompita ikiwa hakusujudu pamoja na imamu.

Swali: Kabla ya salamu au baada yake?

Jibu: Asujudu kabla ya salamu. Kufanya hivo ndio bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22310/حكم-ماموم-فاتته-ركعة-وقام-الامام-لخامسة
  • Imechapishwa: 02/02/2023