Msamaha na uthabiti kwa maiti baada ya kumzika

Swali: Je, ni miongoni mwa Sunnah baada ya kumaliza kumzika maiti mtu awaambie watu:

”Muombeeni ndugu yenu uthabiti”?

Jibu: Ndio. Mfano wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivokuwa akifanya:

”Muombeeni ndugu yenu msamaha na mumuombee uthabiti.”

Swali: Mtu aseme hivo mara moja moja au siku zote?

Jibu: Kinachotambulika ni kwamba alikuwa akisema hivo baada ya kumaliza kumzika maiti.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22312/حكم-قول-اسالوا-لاخيكم-التثبييت-بعد-الدفن
  • Imechapishwa: 02/02/2023