Vipi kuoanisha kati ya makatazo ya kuitwa bwana na yeye mwenyewe kujiita kuwa ni bwana wa wana wa Aadam?

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwakataza Maswahabah waliposema:

”Wewe ni bwana wetu.”

ambapo akasema kuwa Bwana ni Allaah. Vipi tutaoanisha hilo na maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema:

”Mimi ni bwana wa wana wa Aadam na si fakhari”?

Jibu: Aliwaambia hivo ili kusiwapelekei katika kuchupa mpaka. Alichelea juu yao kuchupa mpaka. Aliwaambia:

”Semeni maneno yenu au baadhi ya maneno yenu na wala asikufitinisheni shaytwaan. Kuhusu baada ya kufa kwake hakuna tena…

Jibu: Je, hakuwa akieleza kuwa yeye ni bwana wa wana wa Aadam?

Jibu: Yeye ni kiongozi wa wana wa Aadam. Lakini hakupenda kusifiwa hivo katika uhai wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alichelea juu yao kupetuka mpaka.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22244/الجمع-بين-حديثي-سيد-ولد-ادم-والسيد-الله
  • Imechapishwa: 19/01/2023