Swali: Vipi kuhusu kuwapa zakaah ndugu na jamaa?

Jibu: Hapana neno wakiwa ni mafukara. Lakini asiwape wazazi na kupanda juu, na watoto na kushuka chini. Inafaa akawapa ndugu zake, ami zake na wajomba zake wakiwa ni mafukara. Kuhusu wazazi na watoto hapana.

Swali: Je, inafaa kuwapa zakaah wale wanaojenga misikiti?

Jibu: Hapana. Pesa ya zakaah haijengewi misikiti.

Swali: Vipi ikiwa wanahitaji?

Jibu: Wapewe katika pesa zingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22762/ما-حكم-الزكاة-للاقارب-وبناء-المساجد
  • Imechapishwa: 18/08/2023