Swali: Bwana mmoja alimwambia mshirikina kwamba Allaah hatomwingiza Peponi. Je, huku ni kumuapia Allaah?

Jibu: Asiseme hivo. Amwambie kuwa Allaah hatomwingiza Peponi akifa juu ya shirki. Ambainishie ya kwamba akifa katika shirki basi atakuwa katika watu wa Motoni:

وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ

“Lau wangemshirikisha bila shaka yangeporomoka yale waliyokuwa wakitenda.”[1]

إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ

“Hakika yule atakayemshirikisha Allaah, basi hakika Allaah atamharamishia Pepo na makazi yake yatakuwa ni Motoni.”[2]

[1] 06:88

[2] 05:72

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22765/هل-يجوز-قول-لن-يدخلك-الله-الجنة-للمشرك
  • Imechapishwa: 18/08/2023