Ambao inafaa na wasiofaa kujifunua mbele yao

Swali: Je, mke wa baba mdogo na baba mkubwa ni katika Mahaarim?

Jibu: Mke wa ami sio katika Mahaarim, mke wa mjomba wala mke wa kaka yako. Mke wa ami, mke wa mjomba na mke wa kaka yako sio katika Mahaarim. Haijuzu kujifunua mbele ya mpwa wa mumewe, ndugu wa mumewe wala mwana wa dada wa mumewe. Ni watu kando ambao unalazimika kujisitiri mbele yao.

Ambao ni Mahaarim ni mke wa baba yako na mke wa babu yako. Hawa ni katika Mahaarim. Aidha mke wa mtoto wako wa kiume, mke wa mjukuu wako na mtoto wa msichana wako. Hawa ndio Mahaarim. Wake wa baba na wake wa babu ni haramu. Wake wa watoto wako na wake wa wajukuu zako ni haramu. Kuhusu mke wa baba yako, mke wa ami yako na mke wa mjomba wako hapana.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22751/حكم-وكيفية-اهداء-الثواب-للميت
  • Imechapishwa: 18/08/2023