Ndoa wakati mwanamke ana mimba ya uzinzi

Swali: Mwanaume amemzini mwanamke ambapo akashika ujauzito wa haramu. Kisha mwanaume huyo akaenda kwa baba yake na kuomba kumuoa ambapo akaozeshwa naye. Akamuoa mwanamke akiwa na mimba ya miezi mitatu. Ni ipi hukumu ya ndoa hiyo? Je, inasihi?

Jibu: Ndoa haisihi na ujauzito wa uzinzi mpaka mwanamke atubie na mpaka mwanamke atoke ndani ya eda ya uzinzi huu mbaya na ikauke hedhi yake na atubie. Baada ya hapo ndipo inafaa kwake kumuozesha.

Swali: Ndoa haisihi hata kama ni mwanaume huyohuyo?

Jibu: Hata kama ni mwanaume huyohuyo. Kwa sababu mimba hiyo sio yake. Kwa msemo mwingine ni mimba ya uzinzi na mtoto hatonasibishwa kwake. Jengine ni kwamba mwanamke mzinzi ni lazima atakwe kutubia na yeye mwanaume atubie. Haifai kwake kumuoa isipokuwa baada ya yeye mwanamke kudhihirisha tawbah. Kadhalika mwanaume haendani naye mpaka na yeye adhihirishse tawbah. Kwa hali zote wote wawili wanatakiwa kutubia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22751/حكم-وكيفية-اهداء-الثواب-للميت
  • Imechapishwa: 18/08/2023