Swali: Ni ipi hukumu ya kanuni hii na ni sahihi:

“Yule asiyemfanyia Tabdiy´ mzushi basi yeye ndiye mzushi”?

Jibu: Hakuna shaka yoyote ya kwamba mzushi anatakiwa kuachwa na kususwa mpaka pale atapotubu kwa Allaah (´Azza wa Jall). Lakini ni nani mwenye kuweza kuhukumu ya kwamba huyu ni mzushi? Ni wanachuoni ndio wenye kufanya kazi hii. Leo vijana – Allaah awaogoze – wamekuwa wanawafanyia watu Tabdiy´, bali mpaka kukufurisha bila ya elimu na baswiyrah. Hili halijuzu. Hili linawarejelea wanachuoni wenye kujua Sunnah kutokana na Bid´ah, kufuru na imani na namna ya kutangamana na watu hawa. Wawaulize wao juu ya hayo. Sio kila mtu anafanya Tabdiy´, anasusa na anamzungumzia mwingine bila ya elimu na baswiyrah. Hili halijuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/15216
  • Imechapishwa: 28/06/2020