Kumtoa maiti Ulaya na kwenda kumzika nchi nyingine

Swali: Bibi yangu ameuasia akifa asafirishwe kupelekwa katika nchi yake ya asli. Hivi sasa anaishi Uingereza na yuko katika hali ya mauti. Je, tutakeleze wasia huu?

Jibu: Mzikeni pamoja na waislamu. Uingereza na kwenginepo, kote kuna makaburi ya waislamu. Mzikeni pamoja na waislamu na himdi zote ni za Allaah. Ama katika mji kukiwa hakuna makaburi ya waislamu ndio asafirishwe kupelekwa katika makaburi ya waislamu na asizikwe na makafiri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/15216
  • Imechapishwa: 28/06/2020