Swali: Tunaishi katika mji ambapo tunasumbuka na kukosekana wanachuoni na Ibaadhiyyah kuwa na utawala juu yetu na wanaibania Da´wah ya Salafiyyah na walinganizi wake.

Jibu: Kuweni na subira na mlinganie katika dini ya Allaah (´Azza wa Jall) kwa kiasi na uwezo wenu.

Kuhusiana na kwamba hamna wanachuoni safirini mwende kwa wanachuoni na mjifunze popote wanapopatikana:

فَلَوْلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرْقَةٍ مِّنْهُمْ طَائِفَةٌ لِّيَتَفَقَّهُوا فِي الدِّينِ وَلِيُنذِرُوا قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُوا إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ

“Basi kwanini lisitoke katika kila kundi miongoni mwao, kundi wajifunze dini na ili waonye watu wao watakaporejea kwao ili wapate kutahadhari.” (09:122)

Safirini mwende kutafuta elimu kama jinsi walivyosafiri wanachuoni na maimamu hapo kabla. Safirini mwende kutafuta elimu kwa kadri na mtakavyoweza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/15216
  • Imechapishwa: 28/06/2020