Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

عن أبي هريرة رضي الله عنه أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: (حُجِبَتِ النَّارُ بالشَّهَواتِ، وَحُجِبَتِ الجَنَّةُ بِالمَكَارِهِ). مُتَّفَقٌ عَلَيه

101 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Moto umezungukwa na matamanio. Pepo imezungukwa na mambo yenye kuchukiza.”

al-Bukhaariy na Muslim

Kujiepusha na mambo ya haramu ni jambo lenye kuchukizwa na gumu kwa mioyo. Hivyo ukiulazimisha moyo wako juu ya kuacha mambo haya ya haramu, basi hii ni miongoni mwa sababu za kuingia Peponi.

Tuchukulie lau kuna kijana mwenye nguvu zake anayeishi katika mji wa kikafiri ambapo kuna uhuru ndani yake wa mtu kufanya alitakalo. Mbele yake kuna wanawake na wasichana warembo. Ni kijana mwenye nguvu zake. Bila ya shaka atafikwa na uzito mkubwa wa kuacha uzinifu. Kwa sababu ni jambo sahali kwake na sababu zake ni nyingi. Lakini akiulazimisha moyo wake kuyaacha, basi hii inakuwa ni sababu ya kuingia Peponi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/89-90)
  • Imechapishwa: 14/11/2023