Msafiri aliyesalimika na ajali ya ndege

Allaah (Ta´ala) amesema:

وَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ

“Huenda mkalichukia jambo ilihali ni lenye kheri kwenu.” (02:216)

Tuna uzoefu mwingi wenye kutoa dalili juu ya Aayah hii. Miongoni mwa matukio hayo kuna ndege ilidema ar-Riyaadh na ilikuwa inataka kwenda Jeddah. Ilikuwa imebeba wasafiri wengi. Ilikuwa imebeba zaidi ya wasafiri mia tatu. Kuna msafiri mmoja ambaye alikuwa amebuki kwenda na ndege hii anasubiri kwenye chumba cha wasafiri. Usingizi ukamchukua mpaka akawa amelala. Kukatangazwa  ni muda wa wasafiri kuingia ndani ya ndege na wakaanza kuingia. Ghafla yule mtu aliyekuwa amechukuliwa na usingizi akashtuka baada ya kuwa mlango wa ndege umeshafungwa. Akajuta majuto makubwa nivipi ndege itaweza kumwacha. Baada ya hapo Allaah akakadiria kwa hekima Yake ndege ile ikaungua na wasafiri. Utakasifu ni Wako, ee Allaah! Ni vipi mtu huyu ameweza kusalimika? Amechukia ni vipi ndege inaweza kumwacha lakini hata hivyo hilo likawa ni kheri kwake.

Hivyo basi, wewe utapofanya juhudi na ukamuomba Allaah akusaidie na halafu mambo yakawa kinyume na vile ulivotaka, usijute. Usisemi “Lau ningelifanya kadhaa ingelikuwa kadhaa na kadhaa”. Ukisema hivi unajifungulia mlango wa wasiwasi, majuto na huzuni mkubwa. Mambo yameshapita ipe amani roho yako. Yaegemeze mambo yako kwa Mfalme na Jabbaar (´Azza wa Jall). Badala yake sema:

قدر الله ما شاء فعل

“Ndivyo Allaah alivyopanga. Anachokitaka ndio huwa.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/84)
  • Imechapishwa: 14/11/2023