Swali: Je, bora kwangu ni kusoma Qur-aan au kuswali swalah inayopendeza ninapofika msikitini kabla ya kuadhiniwa?

Jibu: Aswali Raatibah. Kwa mfano Dhuhr kuna Rak´ah nne kabla yake na baina ya kila adhaana na iqaamah kuna swalah. Kukiadhiniwa basi inapendeza kwa walioko msikitini kuswali Rak´ah mbili.

Swali: Wakati mwingine kama mfano wa baada ya Maghrib hakuna Raatibah.

Jibu: Haijalishi kitu aswali Rak´ah mbili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Baina ya kila adhaana mbili kuna swalah. Baina ya kila adhaana mbili kuna swalah.”

Amesema tena:

“Swalini kabla ya Maghrib. Swalini kabla ya Maghrib.”

Kisha akasema:

“Kwa anayetaka.”

Zote hizi ni swalah zinazopendeza baina ya adhaana mbili; Maghrib, ´Ishaa na ´Aswr pia. Kuhusu Dhuhr kuna Raatibah kabla yake. ´Aswr inapendeza kabla yake kuswali Rak´ah nne. Fajr kuna Raatibah kabla yake baina ya adhaana na iqaamah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23031/ماذا-يسن-لمن-حضر-قبل-الاذان-وبعده
  • Imechapishwa: 20/10/2023