Kudumu kunyanyua mikono baada ya swalah za faradhi

Swali: Vipi kuhusu kudumu kunyanyua mikono wakati wa kuomba du´aa baada ya swalah ya faradhi?

Jibu: Si jambo limewekwa katika Shari´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa akinyanyua mikono yake baada ya swalah ya faradhi.

Swali: Kwa hivyo inazingatiwa ni Bid´ah?

Jibu: Haitakikani. Azinduliwe mtu huyo.

Swali: Nikimuona anayefanya hivo?

Jibu: Kama ananyanyua baada ya swalah ya faradhi azinduliwe. Ni jambo lisilofaa. Ni jambo halikuwekwa katika Shari´ah. Bali ni Bid´ah. Akifanya baadhi ya nyakati katika swalah inayopendeza, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya hivo katika swalah inayopendeza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23030/حكم-مداومة-رفع-اليدين-والدعاء-بعد-الفريضة
  • Imechapishwa: 20/10/2023