Uombezi wa Mtume kwa kudumu kuswali shufwa?

Swali: Je, ni kweli kwamba mtu kudumu akiswali shufwa kunapelekea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumuombea anayefanya hivo?

Jibu: Sijui chochote kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya hilo. Muumini anaswali shufwa mchana na usiku. Hii ndio Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah ya usiku na mchana ni [Rak´ah] mbilimbili.”

Witr inakuwa usiku ambayo mtu anamalizia swalah yake kwa Rak´ah moja. Vilevile katika baadhi ya aina ya swalah ya khofu mtu anaswali Rak´ah moja.

Sunnah swalah siku zote inakuwa shufwa isipokuwa Maghrib ambayo ni Witr. Allaah ameifaradhisha Witr kwa Rak´ah tatu. Kuhusu Dhuhr, ´Aswr, ´Ishaa na Fajr zote ni shufwa. Vivyo hivyo swalah zote za kujitolea zinaswaliwa shufwa; Rak´ah mbilimbili. Isipokuwa Witr ndio huswaliwa Rak´ah moja. Kadhalika katika baadhi ya aina ya swalah ya khofu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali Rak´ah moja wakati alipokutana na maadui.

Kuhusu Hadiyth kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali shufwa sijui kuwa ina msingi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/15802/هل-المدوامة-على-صلاة-الشفع-تودي-الى-شفاعة-النبي-ﷺ
  • Imechapishwa: 08/04/2023