Swali: Inafaa katika Ramadhaan kukusanya Maghrib na ´Ishaa na Tarawiyh wakati wa magharibi kukinyesha mvua?

Jibu: Ndio. Kukinyesha mvua, ugumu kwa sababu ya utelezi na utelezi katika masoko, basi bora ni kukusanya kwa ajili ya kuwawepesishia watu. Wakikusanya basi Tarawiyh itaswaliwa baada ya ´Ishaa. Kwa sababu hapo wakati wake utakuwa ni mmoja. Zikikusanywa kati yake katika wakati wa magharibi, basi Tarawiyh itaswaliwa baada yake. Ni sawa kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/15183/حكم-تقديم-صلاة-التراويح-عند-الجمع-لعذر
  • Imechapishwa: 08/04/2023