Swali: Je, kuna Hadiyth inayosema kuwa Witr inaswaliwa kama swalah ya Maghrib?

Jibu: Haikupokelewa. Kinyume chake inachukiza. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuifananisha na Maghrib. Hata hivyo ni sawa akiziswali zote kwa pamoja au akawitirisha kwa Rak´ah moja. Hili la pili ndio bora zaidi. Bora aswali Rak´ah mbili kisha aswali Witr Rak´ah moja. Akiziswali kwa pamoja na akaketi katika ile Rak´ah ya tatu ni sawa. Lakini asiswali kama Maghrib. Inachukiza kufanya hivo. Haitakikani.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/14736/صلاة-الوتر-لا-تصلى-كالمغرب
  • Imechapishwa: 08/04/2023