Mtu kuswali Tarawiyh peke yake nyumbani

Swali: Je, inafaa kwangu kuswali swalah ya Tarawiyh peke yangu?

Jibu: Swalah ya Tarawiyh kwa mkusanyiko ndio bora. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaswalisha Maswahabah zake mkusanyiko nyusiku kadhaa kisha baadaye akaacha kufanya hivo na akasema:

“Mimi nachelea msije kufaradhishiwa swalah ya usiku.”

Alipofariki na Wahy ukasimama ndipo ´Umar aliwakusanya watu nyuma ya imamu mmoja ili awaswalishe ndani ya msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika mwezi wa Ramadhaan. Isitoshe amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika yule atakayesimama pamoja na imamu mpaka akaondoka, basi ataandikiwa ameswali usiku mzima.“

Kwa hivyo bora ni mtu aswali na mkusanyiko kwa ajili ya fadhilah hii kubwa. Lakini hapana vibaya pia ukiswali peke yako nyumbani kwa sababu ni swalah ya kujitolea. Hata hivyo mwenye kuswali na mkusanyiko anapata fadhilah za swalah ya mkusanyiko na pia anapata fadhilah za kusimama usiku mzima akiswali na imamu mpaka mwisho.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/14676/ما-حكم-صلاة-التراويح-بانفراد
  • Imechapishwa: 08/04/2023