Swali: Mimi ni imamu wa msikiti. Wakati mwingine najiliwa na baadhi ya watu na wananiuliza juu ya wanaume ambao wamewaposa wasichana wao. Licha ya kwamba nawajua waposaji vyema, inatokea wakati mwingine nasema kuwa siwajui. Je, inafaa kwangu kufanya hivo?

Jibu: Hapana. Ikiwa unajua kuwa mtu huyu haswali na mkusanyiko [sauti haiko wazi], basi mbainishie jambo hilo kwa sababu amekuomba ushauri. Akikuomba ushauri, basi mshauri. Lakini ikiwa hujui kitu juu ya mposaji, huhitahi kusema chochote. Sema kuwa humjui.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (36)
  • Imechapishwa: 02/09/2023