Zakaah kwa anayestahiki ambaye ameitumia katika haramu

Swali: Bwana mmoja amempa zakaah fakiri anayestahiki kisha baadaye akapata khabari kuwa fakiri huyu ametumia pesa hizo katika mambo ya haramu. Je, inatakasika dhimma yake?

Jibu: Ndio, dhimma yake inatakasika. Kwa sababu amempa mtu ambaye anastahiki. Kitendo cha mtu huyu kuitoa pesa katika mambo yasiyokuwa ya sawa, hilo liko katika dhimma yake yeye, na si dhimma ya yule aliyetoa zakaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (36)
  • Imechapishwa: 02/09/2023