Kitu cha pili ambacho ni kizito kwa watu wengini kunyoa ndevu. Kunyoa ndevu ni haramu.  Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Jitofautisheni na waabudia moto na washirikina. Ziacheni ndevu na punguzeni masharubu.”[1]

Watu wengi nafsi zao zinawashinda na hivo wananyoa ndevu zao. Sijui ni nini wanachofaidika kwa kunyoa ndevu? Hawafaidi lolote isipokuwa maasi yanayomkusanyikia mpaka imani yake inakuwa dhaifu. Miongoni mwa madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kwamba maasi yanaipunguza imani. Kwa kunyoa ndevu unachuma maasi yanayoipunguza imani yako. Pamoja na hivo kitendo hicho hakizidishi uchangamfu [katika ´ibaadah zako], afya wala kukukinga na maradhi. Amepewa mtihani kwa jambo hili na limekuwa zito kwake. Hivyo ni lazima kwa mtu apigane na nafsi yake kwa kutekeleza ya wajibu na kuacha yaliyokatazwa ili awe miongoni mwa wenye kupambana kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall). Allaah (Ta´ala) amesema juu ya malipo yao:

وَالَّذِينَ جَاهَدُوا فِينَا لَنَهْدِيَنَّهُمْ سُبُلَنَا ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ لَمَعَ الْمُحْسِنِينَ

“Na wale waliofanya juhudi kwa ajili Yetu, bila shaka tutawaongoza njia Zetu. Na hakika Allaah yupamoja na watendao wema.” (29:69)

[1]al-Bukhaariy (5892) na Muslim (260 na 259).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/54-55)
  • Imechapishwa: 10/10/2023