Sio kila mwenye kutamkashahaadah damu na mali yake vinasalimishwa. Ni lazima kwa mwenye kuisema atekeleze haki zake. Ndio maana wanachuoni (Rahimahumu Allaah) wamesema lau kutakuwa kijiji miongoni mwa vijiji ambacho kimeacha kuadhini na kukimu, hawakufuru. Lakini hata hivyo wanatakiwa kupigwa vita. Damu yao inakuwa halali mpaka waadhini na kukimu. Pamoja na kuwa adhaana na Iqaamah sio katika nguzo za Uislamu. Lakini hata hivyo ni katika haki za Uislamu. Wamesema vilevle lau wataacha swalah ya ‘iyd ni wajibu kuwapiga vita. Pamoja na kuwa swalah ya ‘iyd sio katika faradhi tano. Wanatakiwa kupigwa vita kwa silaha mpaka waswali pamoja na kuwa swalah ya ‘iyd ni faradhi kwa baadhi ya watu [Fardhw Kifaayah], iliyopendekezwa kwa mujibu wa baadhi ya wanachuoni au faradhi kwa kila mtu [Fardhw ´Ayn] kwa mujibu wa maoni yenye nguvu. Lakini makusudio yetu ni kwamba kupigwa vita kunaweza kujuzu pamoja na kuwa wale wanaopigwa vita ni waislamu ili wadhihirishe zile desturi za Kiislamu za wazi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/48-49)
  • Imechapishwa: 10/10/2023