73. Mwanamke analaamiwa kwa kuyafanya haya

Kwa ajili hiyo Imaam adh-Dhahabiy amesema:

”Miongoni mwa matendo ambayo mwanamke analaaniwa kwayo ni kuonyesha mapambo, dhahabu na lulu chini ya Niqaab, akajitia manukato kwa miski, kaharabu na harufu nzuri wakati anapotoka nje na akavaa nguo za rangirangi, vifungo vya hariri, kofia fupi kwenye kanzu ndefu zenye mikono mirefu na mipana. Yote haya ni katika kujishaua kwa kuonyesha mapambo, jambo ambalo linachukiwa na Allaah na anachukiwa yule mtendaji duniani na Aakhirah. Wanawake wengi wanaingia ndani ya matendo haya ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema juu yake:

”Nimeutazama Moto na kuona wakazi wake wengi ni wanawake.”[1]

Hadiyth ni Swahiyh na ameipokea al-Bukhaariy, Muslim na wengineo kupitia kwa ´Imraan bin Huswayn na wengineo. Ahmad na wengineo wamezidisha kupitia kwa Ibn ´Amr kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”… na matajiri.”

Nyongeza hii cheni yake ya wapokezi ni dhaifu na pia inapingana na mapokezi Swahiyh, kama nilivyobainisha katika ”Silsilat-ul-Ahaadiyth adh-Dhwa´iyfah” (2800).

Uislamu umetilia mkazo kutahadharisha jambo la kujishaua kuonyesha mapambo, kwa kiwango ambacho imeambatanisha jambo hilo na shirki, uzinzi, wizi na mambo mengine ya haramu. Hayo yametajwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa salam) pale alipochukua viapo vya utii kutoka kwa wanawake kwamba wasiingie ndani ya madhambi hayo. ´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

” Umaymah bint Ruqayyah alikuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa salam) kumpa kiapo cha Uislamu. Akasema: ”Kula kiapo kwangu juu ya kwamba hutomshirikisha Allaah na chochote, hutoiba, hutozini, hutowaua watoto wako, hutoleta usingiziaji wa kashfa uliyozua kati ya mikono yako na miguu yako, hutoomboleza na wala hutojishaua kuonyesha mapambo kama walivokuwa wakifanya katika kipindi cha kikafiri hapo mwanzoni.”[2]

[1] Kitaab-ul-Kabaa-ir, uk. 131

[2] Ahmad (02/196) kwa cheni ya wapokezi nzuri. al-Haythamiy amesema:

”Ameipokea at-Twabaraaniy kwa cheni ya wapokezi yenye kuaminika.” (Majma´-uz-Zawaa-id (6/37))

Ameiegemeza kwa at-Twabaraaniy na si Ahmad. Sijui kama kosa ni kutoka kwake au ni wakati wa uchapaji. Katika ”ad-Durr al-Manthuur” (6/209) as-Suyuutwiy ameinasibisha kwa Ahmad na Ibn Marduuyah. Kuna Hadiyth nyingine aliyopokea at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr” kupitia kwa Ibn ´Abbaas.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 120-121
  • Imechapishwa: 10/10/2023