44. Kulipiganwa vita vipi katika mwaka wa 2?

Swali 44: Kulipiganwa vita vipi katika mwaka huo?

Jibu: Vita vya Abwaa´ katika mwezi wa Swafar.

Vita vya Buwaat katika Rabiy´ al-Awwal.

Vita vya ´Ushayrah katika Jumaadaa al-Aakhirah.

Vita vya kwanza vya Badr kisha vita vya Badr vikubwa tarehe 17 Ramadhaan. Kipindi hicho ndipo kuliteremshwa Suurah ”al-Anfaal” yote na kukawekwa katika Shari´ah hukumu zinazohusiana na fai, ngawira na mateka. Waislamu waliohudhuria vita hivyo walikuwa takriban 310.

Vita vya Banuu Sulaym katika mwezi wa Shawwaal.

Vita vya Suwayq katika kumtafuta Abu Sufyaan katika Dhul-Hijjah.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 109-110
  • Imechapishwa: 10/10/2023