al-Aaluusiy amesema:

”Miongoni mwa mapambo yaliyokatazwa kunaingia pia yale ambayo wanawake wa kifahari wa zama zetu hizi wanavaa juu ya nguo zao na wanayojifunika kwayo wakati wanapotoka nje ya majumba yao. Nakusudia kifuniko kilichofumwa kwa hariri ya rangi nyingi na chenye nakshi za dhahabu na fedha zinazoangaza macho. Naona kuwa waume wao na wanaume kama hao wanaowaruhusu kutoka na kutembea namna hiyo kati ya wanamme wa kando ni wakosefu wa wivu, janga ambalo limeenea hivi sasa.

Miongoni mwa mitihani hiyo ni yale yanayofanywa na wanawake wengi ambao hawajisitiri mbele ya mashemeji zao. Vielile waume zao hawajali jambo hilo, licha ya kuwa mara nyingi wamewaamrisha kufanya hivo. Mwanzoni mwanamke hujisitiri mbele yao, lakini tu pale wanapoanza kumpa zawadi ya vito na mfano wake, basi hujiachia na hawajisitiri tena mbele yao. Mambo kama hayo ni miongoni mwa mambo ambayo hayakuidhinishwa na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mifano ya hayo ni mingi.”[1]

[1] Ruuh-ul-Ma´aaniy (6/56).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 121
  • Imechapishwa: 11/10/2023