Tofauti na wanavyodhani wanawake wengi wenye msimamo wa dini sio katika kujishaua kuonyesha mapambo vazi la mwanamke likawa na rangi nyingine isiyokuwa nyeupe au nyeusi. Hilo ni kutokana na sababu mbili:

1 – Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Harufu nzuri ya mwanamke ni ile inayodhihirisha rangi yake na kuficha harufu yake.”[1]

2 – Matendo ya wanawake wa Maswahabah. Nitataja baadhi ya mapokezi yaliyothibiti juu ya hilo kutoka katika ”al-Muswannaf” ya Haafidhw Ibn Abiy Shaybah:

1 – Ibraahiym an-Nakha´iy pamoja na ´Alqamah na al-Aswad walikuwa wakiingia kwa wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuona wamevaa nguo za juu nyekundu.

2 – Ibn Abiy Mulaykah amesema:

”Nilimuona Umm Salamah akiwa amevaa shuka na kanzu ya njano.”

3 – al-Qaasim bin Muhammad bin Abiy Bakr as-Swiddiyq amesema:

”´Aaishah alikuwa akivaa nguo za manjano akiwa katika Ihraam.”

Katika upokezi mwingine imekuja:

”´Aaishah alikuwa akivaa nguo zilizotiwa rangi ya manjano akiwa katika Ihraam.”

4 – Hishaam amesimulia kuwa Faatwimah bint al-Mundhir ambaye amesema:

”Asmaa´ alikuwa akivaa nguo za manjano akiwa katika Ihraam.”

5 – Sa´iyd bin Jubayr ameeleza kuwa aliwaona baadhi ya wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakitufu kwenye Nyumba hali ya kuwa na nguo za manjano[2].

[1] Tazama ”Mukhtaswar-ush-Shamaa-il” (188).

[2] al-Muswannaf (8/371-372).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 121-123
  • Imechapishwa: 11/10/2023