76. Jilbaab ni lazima iwe nzito kiasi cha kwamba haionyeshi mwili

Sharti ya tatu ya jilbaab ni kwamba iwe nzito kiasi kwamba isionyeshe mwili. Kwa sababu sitara haipatikani ikiwa inaonyesha ndani ya mwili. Nguo zinazoonyesha ndani ya mwili zinamzidishia mwanamke fitina na mapambo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mwishoni mwa ummah wangu watakuwepo wanawake waliovaa nguo lakini wako uchi. Vichwa vyao vitakuwa kama nundu ya ngamia. Walaanini, kwani hakika wao ni wenye kulaaniwa.”

Imekuja katika upokezi mwingine:

”Hawatoingia Peponi na wala hawatohisi harufu yake. Hakika harufu yake inahisiwa kutoka umbali wa kadhaa na kadhaa.”[1]

Ibn ´Abdil-Barr amesema:

”Alichokusudia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni wanawake wanaovaa mavazi mepesi yanayoonyesha na wala hayafuniki. Kwa jina ni kwamba wamevaa, lakini ukweli wa mambo ni kwamba wako uchi.”[2]

[1] at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam as-Swaghiyr”, uk. 232, kupitia kwa Ibn ´Amr. Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh. Hadiyth nyingine ameipokea Muslim kupitia kwa Abu Hurayrah. Nimezizungumzia kwa upambanuzi katika ”ath-Thamar al-Mustatwaab”, ”Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah” (1326) na ”Ghaayat-ul-Maraam” (85).

[2] Kutoka katika ”Tanwiyr-ul-Hawaalik” (3/103) ya as-Suyuutwiy. 

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 125-126
  • Imechapishwa: 11/10/2023