Ulazima wa kuosha mikono mara tatu kabla ya kuiingiza ndani ya chombo

Swali: Hadiyth inayosema:

“Anapoamka mmoja wenu kutoka usingizini, basi asizamishe mikono yake ndani ya chombo mpaka kwanza aioshe mara tatu. Kwani hajui mkono wake usiku ulilala wapi.”[1]

Ni kwa njia ya ulazima?

Jibu: Huu ndio msingi. Makatazo yanapelekea katika uharamu na amri inapelekea katika ulazima. Tamko moja linasema:

“Asizamishe… “

Tamko jengine linasema:

“… basi aoshe kwanza mikono yake mara tatu kabla ya  kuiingiza.“

Msingi ni uwajibu.

[1] Ahmad (2/241), al-Bukhaariy (162), Muslim (278), Abu Daawuud (105) na at-Tirmidhiy (24).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23022/هل-حديث-فلا-يغمس-يده-في-الاناء-للوجوب
  • Imechapishwa: 13/10/2023