47. Ni misafara ipi ya kijeshi ilifanyika mwaka wa 3?

Swali 47: Ni misafara ipi ya kijeshi ilifanyika mwaka huo?

Jibu: Katika mwezi wa Jumaadaa al-Aakhirah, Zayd bin Haarithah aliongoza msafara wa kijeshi dhidi ya msafara wa Quraysh na akapata ngawira za vita kutoka hapo.

Katika mwaka huohuo, Muhammad bin Maslamah na Maswahabah wengine wanne walimtokomeza mbali Ka’b al-Ashraf, jambo linalofahamisha kwamba inafaa kufanya hadaa vitani.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 111-112
  • Imechapishwa: 13/10/2023