Ugumu wa kazi au joto kali ni ruhusa ya kumfanya mtu kutokufunga?

Swali: Nilifunga siku ishirini na mbili za Ramadhaan na nikala siku zilizobaki kutokana na hali ya hewa ya joto na kazi ngumu. Nilipe vipi siku nilizokosa?

Jibu: Ni lazima kwako kutubu na kuomba msamaha. Aidha ni lazima kwako kulipa siku zilizobaki. Ni mamoja utafanya hivo kwa kufululiza au kwa kuachanisha. Hapana vibaya kufanya hivo. Kuhusu kazi na joto kali haikuruhusu wewe kula. Unatakiwa kupumzika na kazi na ufunge.

Mwendesha kipindi: Allaah akubariki na akujaze kheri. Wale wanaotoa fatwa kuwa kazi ngumu au joto kali linamruhusu mtu kula?

Ibn Baaz: Hapana, sio udhuru. Yote haya yana ufumbuzi wake; akae mahali ambapo anaona panafaa na apumzike. Siku zilizobaki zinafunika siku hizi zilizosalia na asijihusishe na kazi. Apumzike na kazi, acheleweshe, apunguze au aitengee wakati maalum ambao haumdhuru.

Mwendesha kipindi: Au aihamishe wakati wa usiku?

Ibn Baaz: Au aihamishe wakati wa usiku. Ni vizuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/9627/حكم-من-افطر-اياما-من-رمضان-لمشقة-العمل-وسخونة-الجو
  • Imechapishwa: 28/03/2023