Msafiri kula siku ya kwanza ya Ramadhaan

Swali: Ni ipi hukumu ya msafiri kufunga na kula siku ya kwanza ya Ramadhaan ikimkuta akiwa ndani ya safari yake?

Jibu: Bora kwake ni kula. Akiwa yuko safari basi bora kwake ni yeye kula katika Ramadhaan. Hilo ndio bora. Ni mamoja mwanzoni mwa Ramadhaan au muda mwingine. Bora ni yeye kula. Allaah (Subhaanah) amesema:

وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

”Na atakayekuwa mgonjwa au safarini basi [atimize] idadi katika siku nyinginezo.”[1]

Isitoshe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake walikuwa wakila katika safari na wakati mwingine wakifunga. Jengine ni kwamba Sunnah imefahamisha kuwa bora ni kula. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Si katika wema kufunga safarini.”

[1] 02:185

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/11335/حكم-الفطر-للمسافر-اول-يوم-من-رمضان
  • Imechapishwa: 28/03/2023