Hakuna ulazima wa kulipa swawm inayopendeza aliyofungua mtu

Swali: Nilikuwa nimefunga siku ya jumatatu swawm inayopendeza. Lakini nilipatwa na njaa kali na nikahisi maumivu na uchovu mwingi ambapo dada yangu akanambia nile na kwamba sina dhambi kwa sababu hiyo ni funga inayopendeza, nikafanya hivo. Lakini nimesikia baadhi ya wanawake wakisema kuwa ambaye amekula katika swawm inayopendeza baada ya kufunga sehemu ya siku basi analazimika kulipa. Ni ipi hukumu?

Jibu: Hapana vibaya. Swawm inayopendeza hapana neno kuifungua. Mwenye nayo ndio kiongozi wa nafsi yake; akitaka atakula na ndio bora zaidi, na ikimuia ngumu atafungua na halazimiki kuilipa. Kwa sababu ni swawm inayopendeza na kwa ajili hiyo akitaka ataikamilisha na akitaka pia atakula na hapana vibaya kwake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/12330/حكم-من-افطر-في-صيام-التطوع
  • Imechapishwa: 28/03/2023