Yeyote atakayepinga kufaradhishwa kwa swawm na ulazima wake ni kafiri na ameritadi katika Uislamu. Kwa sababu amepinga faradhi kubwa na nguzo moja wapo miongoni mwa nguzo za Uislamu na kitu kinachotambulika vyema katika dini.

Ambaye atatambua ulazima wa kufunga Ramadhaan na akaacha kufunga kwa makusudi pasi na udhuru, basi amefanya dhambi kubwa ambayo inamfanya kuwa fasiki. Lakini hakufuru kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni. Atalazimishwa kufunga na ataadhibiwa na mtawala wa Shari´ah kwa kufungwa jela, kupigwa mijeledi au yote mawili. Wanazuoni wengine wamesema kuwa akila Ramadhaan bila udhuru basi anakufuru. Tunamuomba Allaah usalama kutokana na kila baya. Pia tunamuomba Allaah uimara juu ya dini yake mpaka wakati wa kufa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ilmaam bishay´ min Ahkaam-is-Swiyaam, uk. 15
  • Imechapishwa: 28/03/2023