al-Fawzaan kuhusu kwenda kwa wanasaikolojia

Swali: Kipindi cha mwisho magonjwa ya akili na wanasaikolojia wamezidi kuwa wengi. Ni jambo linalotambulika kuwa masomo yao hayatokani na Qur-aan na Sunnah. Je, inafaa kwa muislamu anayemtegemea Allaah akawaendea wanasaikolojia hawa kwa ajili ya kujitibisha?

Jibu: Ndio. Jitibisheni na wala msijitibishe kwa kitu cha haramu. Allaah hakuteremsha ugonjwa wowote isipokuwa ameuteremshia dawa. Kujitibitisha hakupingani na kumtegemea Allaah. Hii ni sababu peke yake. Hakupingani na utegemezi wa Allaah. Fanya sababu na umtegemee Allaah. Kusanya kati ya viwili hivyo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/eg–14041434.mp3
  • Imechapishwa: 27/03/2023