Swali: Je, ni lazima kwa mfungaji kukamilisha swawm yake ikiwa analipa siku za Ramadhaan kisha akapenda kufungua na kufanya siku nyingine badala ya siku hii?

Jibu: Kinachotambulika kwa wanazuoni ni kwamba anayeanza jambo la faradhi basi analazimika kulikamilisha na kwamba haijuzu kufungua isipokuwa kutokana na sababu. Sababu hiyo inaweza kuwa maradhi yaliyomsibu, safari au jambo lililozuka. Kwa maana nyingine ni lazima kwake kukamilisha swawm yake ya faradhi kama mfano wa deni la Ramadhaan na nadhiri. Swawm kama hizi anapaswa kuzikamilisha na asifungue isipokuwa kutokana na sababu inayomruhusu kufungua.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1247/حكم-من-شرع-في-صيام-القضاء-ثم-اراد-ان-يفطر
  • Imechapishwa: 28/03/2023