Swali: Siku moja nilikuwa nimefunga swawm ya kulipa na baada ya Dhuhr nikahisi njaa ambapo nikala na kunywa kwa kukusudia pasi na kusahau wala ujinga. Ni ipi hukumu ya kitendo changu?

Jibu: Ni lazima kwako kukamilisha swawm. Haijuzu kula ikiwa swawm hiyo ni ya faradhi kama mfano wa swawm ya Ramadhaan na swawm ya nadhiri. Vilevile ni lazima kwako kutubu kutokana na uliyoyafanya. Anayetubu basi Allaah anamsamehe.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/12447/حكم-قطع-صوم-القضاء
  • Imechapishwa: 28/03/2023