Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye ameenda katika Jihaad pasi na wazazi wake kujua na akafa shahidi. Je, anaingia ndani ya hukumu ya ambaye amepambana jihaad katika njia ya Allaah?

Jibu: Tunataraji kwake hivo – Allaah akitaka. Tunataraji kwake hivo. Tunataraji awe amekufa shahidi na mwenye kusamehewa. Kwa sababu kwenda kwake pasi na idhini ya wazazi juu ya jihaad ni kupenda kwake mambo ya kheri. Kuwaomba idhini wazazi wawili ndani yake kuna mushkili katika jambo kama hili. Tunataraji kwake ujira mkubwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdil-´Aziyz bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4272/حكم-من-ذهب-للجهاد-دون-علم-والديه-واستشهد
  • Imechapishwa: 04/06/2022