Swali: Ni yepi maoni yako kuhusu kutengeneza filamu zinazobeba fikira za Kiislamu ambazo zinaziba pengo lilipo sasa na linalotumiwa hivi sasa kwa filamu ambazo ni chafu?

Jibu: Nimeulizwa swali hili mara nyingi na maoni yanayosema kufaa ni maoni yenye nguvu. Lengo ni ili ziweze kuzuia filamu nyinginezo au kwa kufanya hivo kutokee upunguaji, kuzipiga vita na kupambana nazo. Filamu za kiislamu ambazo zinawaonyesha watu yale yanayowanufaisha katika dini yao, zinawashaji´isha katika kheri na kuwaita katika haki ili ziweze kupiga vita filamu chafu. Sioni ubaya wake kutokana na vile ilivyopelekea dharurah. Kwa sababu watu hivi sasa wanahitaji filamu nzuri ili ziweze kupiga vita filamu chafu ambazo watu wamepewa mtihani kwayo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdil-´Aziyz bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4059/حكم-عمل-افلام-اسلامية-بديلة-عن-الفاسدة
  • Imechapishwa: 04/06/2022