Swali: Ambaye ameingia msikitini akamkuta imamu anatoa Khutah aketi chini na kusikiliza Khutbah au aswali Rak´ah mbili?

Jibu: Kilichowekwa katika Shari´ah ni yeye kuswali Rak´ah mbili kisha aketi chini. Aanze kuswali. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anapokuja mmoja wenu na imamu anatoa Khutbah basi aswali Rak´ah mbili na azikhafifishe.”

Hivi ndivo alivyoamrisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hivyo aanze kuswali kisha aketi chini.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdil-´Aziyz bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4286/ما-المشروع-لمن-دخل-المسجد-والامام-يخطب
  • Imechapishwa: 04/06/2022