Kuna hekima gani mwenye hedhi kulipa swawm na halipi swalah?

Swali: Kuna hekima gani mwenye hedhi kulipa swawm na halipi swalah?

Jibu: Mosi ni kwamba inatambulika kuwa kilicho cha lazima kwa muislamu ni yeye kutekeleza yale maamrisho yote aliyoyawajibisha Allaah na kujiepusha na yale yote ya haramu aliyokataza. Ni mamoja amejua hekima ya maamrisho hayo au hakujua. Sambamba na hayo anatakiwa kuamini kuwa Allaah haamrishi ´ibaadah yoyote isipokuwa ni kutokana na manufaa kwao na hakuwakataza isipokuwa ni kutokana na yale madhara yanayopatikana kwao. Mambo yote yaliyowekwa katika Shari´ah (Subhaanah) ni kutokana na hekima anayoijua Yeye (Subhaanah). Huonekana hekima hiyo kwa waja Wake kwa yale Anayotaka ili kwa jambo hilo imani ya muumini iweze kuzidi na anapendelea (Subhaanah) kwa yale Anayoyataka ili vivyo hivyo imani ya muumini na kujisalimisha kwake kwa Allaah kuzidi.

Pili ni jambo linalojulikana kwamba swalah ni nyingi na ni zenye kukariri mchana na usiku mara tano kwa siku. Hivyo inakuwa ni vigumu kwa mwenye hedhi kuzilipa. Hilo ni tofauti na swawm ambayo inalazimika ndani ya mwaka mara moja. Pengine hedhi ikajitokeza mara moja au mara mbili. Allaah amesema kweli:

يُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُخَفِّفَ عَنكُمْ ۚ وَخُلِقَ الْإِنسَانُ ضَعِيفًا

“Allaah anataka kukukhafifishieni, kwani mtu ameumbwa dhaifu.” (04:28)

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

´Abdullah bin Qu´uud

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (05/437) nr. (2443)
  • Imechapishwa: 04/06/2022