Tunaamini pia kuwa Allaah ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona. Anasikia kila tunachokisema hata kama kitakuwa kidogo. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

أَمْ يَحْسَبُونَ أَنَّا لَا نَسْمَعُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَاهُم ۚ بَلَىٰ وَرُسُلُنَا لَدَيْهِمْ يَكْتُبُونَ

“Au wanadhania kwamba Sisi hatusikii siri zao na minong’ono yao? Sivyo! [tunasikia]na wajumbe wetu wako kwao wanaandika.” (43:80)

يَعْلَمُ السِّرَّ وَأَخْفَى

“.. Yeye anajua ya siri na yanayofichika zaidi.” (20:07)

bi maana kilichofichikana zaidi kuliko siri. Hichi ni kile ambacho mtu anajiambiza ndani ya nafsi yake. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ وَنَعْلَمُ مَا تُوَسْوِسُ بِهِ نَفْسُهُ

“Hakika Tumemuumba mtu na tunajua yale [yote] yanayomshawishi nafsi yake.” (10:16

Kilichomo ndani ya nafsi Allaah anakijua hata kama hakijajidhihirisha kwa mja.

Vilevile Allaah (´Azza wa Jall) ni Mwenye kuona. Anamuona mdudu mchungu mweusi, kwenye mwamba mweusi na kwenye usiku wenye giza. Mdudu mchungu huyo hafichikani kwake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/436-437)
  • Imechapishwa: 12/06/2023