19. Kitu ambacho mlinganizi anatakiwa kulingania kwacho

3 – Kubainisha jambo linalolinganiwa kwalo.

Kitu ambacho kinalinganiwa kwacho na ni lazima kwa walinganizi kuwawekea nacho watu wazi, kama ambavo walifanya Mitume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ni kulingania katika njia ya Allaah ilionyooka; nayo ni Uislamu na ni dini ya Allaah ya haki. Hapa ndipo pahala pa ulinganizi. Allaah (Subnaanah) amesema:

ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ

“Lingania katika njia ya Mola wako… ”

Njia ya Allaah (Jalla wa ´Alaa) ni ule Uislamu, njia ilionyooka na ndio ile dini ya Allaah ambayo amemtuma kwayo Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hiki ndicho ambacho ni lazima kulingania kwacho. Mtu asilinganie katika madhehebu fulani wala maoni ya fulani. Lakini katika dini ya Allaah na njia ya Allaah ilionyooka ambayo Allaah amemtumiliza nayo Mtume Wake na kipenzi chake wa hali ya juu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hayo ni yale yaliyojulishwa na Qur-aan tukufu na Sunnah takasifu na zilizothibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Katika kilele yake ni kulingania katika ´Aqiydah sahihi, kumtakasia nia Allaah, kumpwekesha kwa ´ibaadah, kumwamini Yeye, Mitume Yake, siku ya Mwisho na kila ambacho ameeleza Allaah na Mtume Wake. Huu ndio msingi wa njia ilionyooka. Nako ni kulingania katika kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Maana yake ni kulingania katika kumwabudu Allaah pekee, kumtakasia Yeye nia, kumwamini Yeye na Mitume Yake (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Da´wah ilaa Allaah wa Akhlaaq-id-Du´aah, uk. 30-31
  • Imechapishwa: 12/06/2023