18. Madhara ya ulinganizi wa ujinga ni mkubwa zaidi

Kulingania kwa ujinga ni kitu kinadhuru na wala hakinuifaishi. Hilo tutalibainisha – Allaah akitaka – wakati tutataja tabia za walinganizi. Kulingania pamoja na dalili kwa dalili ni kumsemea Allaah pasi na elimu. Vivyo hivyo kulingania kwa ukali na ususuwavu madhara yake ni makubwa zaidi. Kilicho cha lazima na kilichowekwa katika Shari´ah ni kufanyia kazi yale aliyoyabainisha Allaah (´Azza wa Jall) katika Suurah “an-Nahl”. Amesema (Subhaanah):

ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ

“Lingania katika njia ya Mola wako kwa hekima… ”

Isipokuwa kukionekana kutoka kwa yule anayelinganiwa ukaidi na dhuluma. Katika hali hiyo ni sawa kumfanyia ukali. Allaah (Subhaanah) amesema:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ جَاهِدِ الْكُفَّارَ وَالْمُنَافِقِينَ وَاغْلُظْ عَلَيْهِمْ

“Ee Nabii! Fanya jihaad dhidi ya makafiri na wanafiki na kuwa mkali kwao.”[1]

وَلَا تُجَادِلُوا أَهْلَ الْكِتَابِ إِلَّا بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ إِلَّا الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْهُمْ

“Na wala msijadiliane na Ahl-ul-Kitaab isipokuwa kwa yale ambayo ni mazuri zaidi; isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao.”[2]

[1] 09:73

[2] 29:46

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Da´wah ilaa Allaah wa Akhlaaq-id-Du´aah, uk. 28-29
  • Imechapishwa: 12/06/2023