Kuna watu waliyopotea upotevu mkubwa kabisa pale ambapo walipinga kuwepo kwa Malaika. Wamesema kuwa Malaika ni ibara kuhusu kheri yenye nguvu. Wamesema kuwa hakuna kitu kinachoitwa ulimwengu wa Malaika.

Watu hawa ikiwa ni wenye kupindisha maana, basi lililo la wajibu ni kuwabainishia kuwa kitendo hichi ni batili bali ni upotoshaji. Wakipinga pasi na kupindisha maana, basi ni makafiri. Kwa sababu wamekadhibisha yaliyotajwa ndani ya Qur-aan, Sunnah na Ummah ukaafikiana kwalo juu ya uwepo kwa Malaika.

Allaah ni muweza kuumba ulimwengu mzima na binadamu asiuhisi kwa njia waliyozowea ya akili. Majini wapo na ni jambo lisilokuwa na shaka juu ya uwepo wao. Pamoja na hivyo akili zetu za dhahiri haziwahisi kama jinsi tunavyohisi vitu vingine vilivyoko dhahiri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/445-446 )