Tende tosa, tende za kawaida, maji au chengine chochote

Swali: Mtu akate swawm kwa maji na tende au chochote kingine?

Jibu: Kwa chochote kitachomuwepesikia. Lakini bora ni kwa tende. Tende tosa ndio bora zaidi, kisha tende za kawaida halafu maji. Hapana vibaya pia akikata swawm kwa mkate au kitu kingine.

Swali: Akikata swawm kwa kitu kingine?

Jibu: Hapana vibaya. Lakini bora ni kwa tende tosa au tende za kawaida. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Afutari kwa tende, kwani zina baraka. Asipopata, basi afutari kwa maji, kwani ni yenye kutwahirisha.”

Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifutari kwa tende tosa, asipopata akifutari kwa tende, asipopata anafutari kwa glasi ya maji.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22805/حكم-الافطار-على-غير-التمر-او-الماء
  • Imechapishwa: 24/03/2023