Swali: Nilikula Ramadhaan nikiwa ´Iraaq kwa sababu ya kazi inayonifanya kuweza kuwahudumia watoto wangu. Lakini naweza kulipa wakati nitaporudi Misri. Ni ipi hukumu?

Jibu: Muda wa kuwa umenuia kukaa ´Iraaq kwa sababu ya kazi ni lazima kwako kufunga. Ikiwa umenuia kufunga Ramadhaan au zaidi ya Ramadhaan ukiwa ´Iraaq au kwenginepo, basi ni lazima kwako kufunga na wengine. Hauna udhuru wa kuacha kufunga. Haya ndio maoni ya kikosi kikubwa cha wanazuoni. Ni lazima kwako kufunga na huna hukumu moja kama msafiri. Bali unapaswa kufunga na wengine. Ukifikwa na kikwazo kama vile ugonjwa au ukasafiri katikati ya Ramadhaan, basi una ruhusa ya kula kutokana na safari au maradhi. Lakini muda wa kuwa ni mkazi na unafanya kazi, ni lazima kwako kufunga na wengine. Haifai kwao kula. Kwa sababu uliacha kufunga pasi na udhuru wa safari au ugonjwa basi ni lazima kwako kutubu kwa Allaah na ni lazima kwako kulipa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/8095/الافطار-في-رمضان-بحجة-العمل
  • Imechapishwa: 24/03/2023