Tayammum haichenguki kwa kumalizika wakati

Mtu akikosa maji na bado akawa yuko na wudhuu’, Tayammum inachukua mahali pa maji na Tayammum yake haichenguki kwa kumalizika wakati wa swalah. Kwa mfano lau mtu atafanya Tayammum kwa ajili ya Dhuhr ilihali ni msafiri na hana maji, na akabaki na asipate hadathi mpaka ´Ishaa sio lazima kwake kurudi kufanya Tayammum kwa mara nyingine. Tayammum haivunjiki kwa kutoka kwa wakati. Tayammum ni twahara inayokubalika kwa mujibu wa Shari´ah. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ ۚ مَا يُرِيدُ اللَّـهُ لِيَجْعَلَ عَلَيْكُم مِّنْ حَرَجٍ وَلَـٰكِن يُرِيدُ لِيُطَهِّرَكُمْ

“… panguseni kwayo nyuso zenu na mikono yenu. Allaah hataki kukufanyieni magumu, lakini anataka kukutwahirisheni.”(05:06)

Allaah amebainisha kuwa Tayammum ni twahara. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ardhi yote imefanywa kwangu kuwa ni mahali pa kuswalia na safi… “

Bi maana yenye kutwahirisha.

“… yeyote katika Ummah wangu aswali pale ambapo swalah itapomkuta.”[1]

Katika Hadiyth nyingine imekuja:

“Hapo alipo ndio mahala pake pa kuswalia na twahara yake.”[2]

Bi maana ajitwahirishe na kuswali.

[1] al-Bukhaariy (438).

[2] Ahmad (05/248).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/365-366)
  • Imechapishwa: 16/05/2023