33. Tunatakiwa kama walivofanya Salaf

Miongoni mwa mambo yasiyokuwa na shaka yoyote ni kwamba njia zilizowekwa katika Shari´ah ndizo ambazo Allaah kwazo amewaongoza waarabu katika Uislamu na ndizo njia ambazo zilitumiwa na zile karne bora. Aidha ndio msingi wa Salafiyyah yote ilioenea ulimwenguni. Njia hizo zilizosuniwa ni zenye kutosheleza kuilea jamii iweze kutendea kazi Uislamu kama ilivyokuwa hapo mwanzoni. Ndio maana Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walikuwa ni wenye kupupia zaidi kushikamana na njia hizi na wenye kukemea zaidi njia zote mpya zinazozuliwa. Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema:

“Tunaona kuwa misingi ya Sunnah ni kushikamana na yale waliyokuwemo Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuwaigiliza na kuacha Bid´ah na kila Bid´ah ni upotofu.”[1]

al-Awzaa´iy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Isubirisheni nafsi yako juu ya Sunnah, simama pale waliposimama watu, sema kila walichokisema na jiepushe na kile walichojiepusha. Fuata njia ya watangu wako wema. Kwani kitakutosha kile kilichowatosha.”[2]

Ikiwa zile njia za kulingania zilizowatosha Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) haziwatoshi baadhi ya wale wanaojiita ni walinganizi, basi ni lazima iwe ni moja kati ya mambo mawili:

1 – Ima wao ni waongofu zaidi kuliko Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

2 – Au watakuwa wamekuja na Bid´ah zenye kupotosha.

Kila kimoja katika hayo mawili ni kikubwa. Kwa ajili hiyo hebu walinganizi wahakikishe wameshikana na zile njia zilizowatosheleza Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Walikuwa wakifanya mambo yao kwa elimu.

[1] Usuul-us-Sunnah.

[2] Talbiys Ibliys, uk. 9, ya Ibn-ul-Jawziy.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 40-41
  • Imechapishwa: 16/05/2023